Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake?
Mkariri:Kevin Kogo
Yule aliyesema haezi kubabaishwa na mapenzi
Alikutwa amejinyonga na barua ndefu ya malalamiko ya kusalitiwa!
Yule bwana mdogo aliyekua akiamini mtu mzima hakosei
Leo amezeeka na ujinga wake!
Yule kasisi aliyeshinda akiubiri kuhusu heshima na ndoa
Jumamosi hii ilimkuta kafumaniwa lodging na mke wa mtu!
Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake?
Mwalimu aliyetufundisha vyema swala la unyanyasaji wa kijinsia
Nyumbani kwake haipiti siku bila kumpiga mkewe!
Mchawi na macho yake mekundu kuwakemea na kuwaroga wengine
Leo amefiwa analia dunia haina huruma!
Yule binti aliyemsifu mamake kwa kumlea japo ya shida na taabu
Historia inamhukumu kwa kutoa mimba tatu sababu uoga wa malezi!
Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake?
Bi Mkubwa aliyekua akimkejeli bi mdogo sababu ya tatizo la ugumba
Leo analia watoto wake wamefariki kwa ajali ya moto na ndoa yake inateketea!
Aliyemtenga rafiki yake baada ya kufeli mitihani
Leo yuko kwenye foleni ya kuajiriwa kazi akitangaza bosi amesoma naye!
Jaji aliyemhukumu mtu bila ushaidi kwa hongo wa mlango wa nyuma
Leo yupo ndani akilalamika sio kila mtu jela anahatia!
Aliyeshinda akitangaza mtoto wa jirani Malaya
Leo yupo kitandani kaswende inamshambulia maungo yake!
Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake?
Walimwengu ni mwalimu katili , sarafu ya maisha haitabiriki .
Comments
Post a Comment