Posts

Showing posts from September, 2024

Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake?

Image
  Mkariri:Kevin Kogo Yule aliyesema haezi kubabaishwa na mapenzi Alikutwa amejinyonga na barua ndefu ya malalamiko ya kusalitiwa! Yule bwana mdogo aliyekua akiamini mtu mzima hakosei Leo amezeeka na ujinga wake! Yule kasisi aliyeshinda akiubiri kuhusu heshima na ndoa Jumamosi hii ilimkuta kafumaniwa lodging na mke wa mtu! Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake? Mwalimu aliyetufundisha vyema swala la unyanyasaji wa kijinsia Nyumbani kwake haipiti siku bila kumpiga  mkewe! Mchawi na macho yake mekundu kuwakemea na kuwaroga wengine Leo amefiwa analia dunia haina huruma! Yule binti aliyemsifu mamake kwa kumlea japo ya shida na taabu Historia inamhukumu kwa kutoa mimba tatu sababu uoga wa malezi! Nani hajawahi kuishi Njee ya maneno yake? Bi Mkubwa aliyekua akimkejeli bi mdogo sababu ya tatizo la ugumba Leo  analia watoto wake wamefariki kwa ajali ya moto na ndoa yake inateketea! Aliyemtenga rafiki yake  baada ya kufeli mitihani Leo yuko kwenye foleni y...